99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

AfDB yaahidi kuunga mkono marekebisho ya mfumo wa madeni nchini Zambia

(CRI Online) Julai 19, 2023

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana imeahidi kuiunga mkono Zambia baada ya nchi hiyo kufikia makubaliano na wadeni wake rasmi juu ya kupanga upya utaratibu wa madeni.

Akizungumza alipokutana na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema mjini Lusaka, Rais wa Benki hiyo Akinwumi Adesina amesema, Benki yake inafikiria machaguo mbalimbali katika kuiunga mkono Zambia, ikiwemo kuboresha uwezo wa nchi hiyo wa kujadili madeni yake kufuatia mchakato wa upangaji mpya wa madeni hayo.

Kwa upande wake, Rais Hichilema ameishukuru AfDB kwa kuiunga mkono, na kutoa wito kwa msaada zaidi kufuatia nchi hiyo kuingia kwenye awamu ya majadiliano na wadeni wake kutoka sekta binafsi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha