WFP yasema watu milioni 2.7 wakimbia makazi yao kutokana na ukame katika Pembe ya Afrika
(CRI Online) Julai 17, 2023
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema, hali ya ukame katika eneo la Pembe ya Afrika imesababisha watu milioni 2.7 kukimbia makazi yao.
Ripoti ya WFP iliyotolewa jana imesema, watu milioni 1.7 nchini Somalia, watu 516,000 nchini Ethiopia na watu 466,000 nchini Kenya wamekimbia makazi yao kutokana na ukame.
Ripoti hiyo pia imesema kuwasili kwa maelfu ya wakimbizi katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame katika nchi hizo tatu kunazidisha uhaba wa chakula katika kanda hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma