99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yatoa vifaa vya michezo kwa Tanzania ili kuhamasisha vipaji vya vijana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2023

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Pindi Chana wakionyesha vifaa vya michezo kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 10, 2023. China imetoa vifaa vya michezo kwa Tanzania siku ya Jumatatu ili kuhamasisha vijana kuendeleza vipaji vyao. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

DAR ES SALAAM - China imekabidhi vifaa vya michezo kwa Tanzania siku ya Jumatatu ili kuhamasisha vijana kuendeleza na kukuza vipaji vyao.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na Idara Kuu ya Michezo ya China kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania vitagawiwa kwa shule mbili nchini Tanzania.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Pindi Chana ameishukuru serikali ya China kwa msaada huo ambao amesema utasaidia sana katika kukidhi mahitaji ya nchi hiyo katika sekta ya michezo.

“Kwa vifaa hivi, tunaamini vijana wetu wataweza kuinua vipaji vyao vya michezo, jambo ambalo litawezesha taifa letu kuwaandaa wanataaluma wengi wa michezo,” amesema Chana kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika Uwanja wa Taifa wa Tanzania, jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema mawasiliano kati ya China na Tanzania katika michezo yamekuwa na mchango chanya katika kukuza maelewano kati ya watu wa China na Tanzania.

"Tuungane mkono kuuleta ushirikiano wa nchi mbili katika michezo kwenye ngazi ya juu zaidi katika siku zijazo," balozi huyo wa China amesema.

Wanamichezo wa Tanzania wakiangalia vifaa vya michezo vilivyotolewa na China kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 10, 2023. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

Wanamichezo wa Tanzania wakiangalia vifaa vya michezo vilivyotolewa na China kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 10, 2023. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha