99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wanafunzi wa Kenya wenye matumaini makubwa waweka malengo ya kuendelea kusoma nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2023

Wanafunzi wakitembelea Stesheni ya mwisho ya Reli ya Nairobi, Kenya, Julai 8, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

Wanafunzi wakitembelea Stesheni ya mwisho ya Reli ya Nairobi, Kenya, Julai 8, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

NAIROBI - Kundi la wanafunzi 52 wa Kenya, ambao wametuma maombi ya kuomba ufadhili wa masomo kwa serikali ya China, wamemaliza semina ya siku mbili katika mji wa bandari wa Mombasa siku ya Jumapili, huku washiriki wakieleza nia yao ya kuhimiza urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Mwishoni mwa wiki, wanafunzi hao walitembelea Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Nairobi, na Afristar, kampuni inayoendesha Reli ya Standard Gauge (SGR), miradi miwili mikuu inayohusiana na ushirikiano kati ya China na Kenya.

Maafisa kutoka Wizara ya Elimu ya Kenya, Ubalozi wa China nchini Kenya, na Shirikisho la Wahitimu wa masomo wa Kenya waliosoma China pia walishiriki majadiliano kwenye semina hiyo.

Wanafunzi hao ambao wanatarajia kuendelea na masomo yao katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China wameapa kutumia fursa hiyo kikamilifu na kuwa wajumbe wa urafiki kati ya nchi hizo mbili ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo ulio wa udhati, wenye matokeo halisi, upendo na nia njema.

Darius Mogaka Ogutu, mkurugenzi wa elimu ya juu katika Wizara ya Elimu ya Kenya, amesema anashukuru serikali ya China kwa kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kenya.

"Hii ni fursa kwenu kung'ara, kwa nyie kuweza kurejea na kushiriki (yale mliyojifunza), na kujenga nchi yenu na kuwatia moyo watu wengi zaidi," Ogutu amesema.

Picha hii, iliyopigwa Julai 9, 2023, inaonyesha semina ya wanafunzi ikifanyika mjini Mombasa, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

Picha hii, iliyopigwa Julai 9, 2023, inaonyesha semina ya wanafunzi ikifanyika mjini Mombasa, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

Kwenye semina hiyo, Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian aliwaambia wanafunzi hao kwamba kuelewa dhana ya China inayojikita kwa umma kutawasaidia kwa kiasi kikubwa kuelewa nchi hiyo na kuendelea na masomo yao vyema.

Akisisitiza urafiki wa kudumu kati ya China na Kenya, Zhou amesema kila mwanafunzi wa Kenya nchini China ni mjumbe wa mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili.

Jacob Oloo, ni mmoja wa wanafunzi hao ambaye ametuma maombi ya ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamivu (PhD) katika teknolojia ya habari kwenye vyuo vikuu kadhaa katika mji mkuu wa China, Beijing.

Akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Mombasa Oloo amesema "Siku zote ni vizuri kuwa sehemu ya maendeleo ya China."

Jacob Oloo, ambaye ametuma maombi ya ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamivu (PhD) katika teknolojia ya habari kwenye vyuo vikuu mbalimbali katika mji mkuu wa China, Beijing, akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Mombasa, Kenya, Julai 9, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha