99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kampuni 18 za Zambia kushiriki Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2023

LUSAKA - Jumla ya kampuni 18 za Zambia zimefuatana na ujumbe wa serikali kushiriki Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yaliyopangwa kuanza leo Juni 29 huko Changsha, Mkoa wa Hunan, China, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zambia Chipoka Mulenga amesema Jumatano.

Mulenga amesema kampuni zinazojihusisha na sekta mbalimbali ikiwemo madini, madini ya vito, mbao na uvuvi pamoja na nyinginezo zimeambatana naye katika maonyesho hayo.

Amesema katika taarifa yake kuwa Zambia iko tayari kujifunza mbinu nzuri za biashara na viwanda kutoka nchi zilizoendelea kiteknolojia kama China.

Ameongeza kuwa hakuna nchi yoyote duniani ambayo imeweza kuendelea kiuchumi bila kuwashirikisha wananchi wake kupitia ubia, na kwa muda mrefu amekuwa akitoa wito kwa Wazambia kujihusisha hasa katika uongezaji thamani.

Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yaliyozinduliwa kwa mara ya kwanza Mwaka 2019 ni jukwaa kuu la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha