99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

UNHCR yasema wakimbizi zaidi ya milioni 2.4 watahitaji kupata makazi mapya katika Mwaka 2024

(CRI Online) Juni 27, 2023

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) jana Jumatatu limesema, zaidi ya wakimbizi milioni 2.4 watahitaji kupata makazi mapya katika kipindi cha Mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na idadi ya Mwaka 2023.

Kutokana na ripoti ya tathmini kuhusu Makadirio ya Mahitaji ya Makazi Mapya Duniani, Asia iko nafasi ya kwanza katika orodha ya mahitaji ya Mwaka 2024 ikiwa na wakimbizi karibu 730,000 watakaohitaji kupata makazi mapya, ikichukua asilimia 30 ya idadi ya jumla ya mahitaji ya dunia nzima.

Kutokana na kuendelea kwa mgogoro wa Syria, wakimbizi 754,000 wanahitaji kupata msaada wa dharura kwa kupitia kupewa makazi mapya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha