99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

FAO yazindua mradi wa kuzuia kuzaliana na kusambaa kwa viwavijeshi Mashariki mwa Afrika

(CRI Online) Juni 16, 2023

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Alhamisi lilizindua mradi katika mji wa Naivasha nchini Kenya ili kulinda mazao ya chakula kutokana na hasara kubwa inayosababishwa na viwavijeshi, wadudu ambao wanaweza kuharibu hadi asilimia 100 ya vyakula vikuu kama wataachwa bila kudhibitiwa.

Mradi huo, unaojulikana kama Usaidizi wa Dharura wa Kudhibiti Milipuko na Uvamizi wa Viwavijeshi Mashariki mwa Afrika, unalenga kutumia uwezo wa kitaifa katika eneo la Mashariki mwa Afrika dhidi ya uvamizi wa wadudu hao.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Uzalishaji na Ulinzi wa Mimea katika FAO Xia Jingyuan, amesema wadudu hao ni tishio kubwa la kusababisha uhaba wa chakula katika eneo hilo, na hivyo kulazimisha uingiliaji kati wa haraka wa FAO na washirika wake ili kuzuia upotezaji mkubwa wa mazao, ambayo tayari yamepungua kutokana na shinikizo la ukame wa muda mrefu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha