99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Biden atoa amri ya kupandisha bendera nusu mlingoti baada ya shambuzili la bunduki la Texas

(CRI Online) Mei 08, 2023

Habari kutoka Ikulu ya Marekani imesema, Rais Joe Biden ametoa amri ya kupandisha bendera ya nchi hiyo nusu mlingoti baada ya shambuzili la bunduki lililotokea jimboni Texas.

Mashambulizi matatu mfululizo yalitokea Ijumaa na Jumamosi nchini Marekani, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 11 na wengine wengi kujeruhiwa. Shambulizi moja lilitokea katika soko kubwa jimboni Texas Jumamosi mchana na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine saba kujeruhiwa. Jingine lilitokea Jumamosi alfajiri kwenye sherehe iliyofanyika nyumbani jimboni California, ambapo msichana mmoja aliuawa na wengine watano kujeruhiwa. Aidha katika shambulizi la tatu lililotokea Ijumaa usiku katika mgahawa ulioko jimboni Mississippi, limesababisha mtu mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa.

Biden ametoa taarifa akisema Ikulu ya Marekani inafuatilia kwa makini hali ya mashambulizi, na kuwasiliana na idara ya kusimamia utekelezaji wa sheria na maofisa wa majimbo ili kutoa msaada.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha