99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wakurugenzi wa Afya barani Afrika watoa wito wa uwekezaji katika utambuzi ili kudhibiti magonjwa barani humo

(CRI Online) April 28, 2023

Wakurugenzi wa afya kutoka nchi za Afrika wamesema, ongezeko la magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza barani Afrika unaweza kudhibitiwa mara bara hilo litakapotoa kipaumbele katika uwekezaji wa vifaa vya kisasa vya ugunduzi.

Naibu Mkuu wa kampuni ya kimataifa ya kutengeneza dawa ya Roche Diagnostic Afrika, Allan Pamba amesema, maboresho katika vifaa vya vipimo vya malaria, VVU na UKIMWI, homa ya manjano, magonjwa ya moyo, kisukari na saratani yataboresha tiba zake na huduma huku yakipunguza idadi ya vifo kwa wagonjwa.

Kaimu Mkuu wa kampuni hiyo katika nchi zinazozungumza Kiingereza Kanda ya Afrika Magharibi, Taofik Oloruko-Oba, amesisitiza kuwa, mtazamo mpya kwa ajili ya miundombinu inayofaa ya utambuzi katika taasisi za afya barani Afrika unatakiwa ili kukabiliana na magonjwa unaohusishwa na mtindo mbaya wa maisha.

Naye Mkurugenzi wa Mageuzi ya Mkakati na Huduma za Afya wa kampuni hiyo barani Afrika, Jonathan Ketel amesema, nchi za Afrika zinapaswa kuwekeza katika vifaa vya utambuzi ili kuboresha vipimo vya magonjwa kama sehemu ya ajenda ya kimataifa ya afya kwa wote.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha