China kuendelea kutoa mchango kusaidia nchi za Kiarabu kufikia umoja
(CRI Online) April 14, 2023
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw.Wang Wenbin amesema, China iko tayari kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuzisaidia nchi za Kiarabu kufikia umoja.
Bw.Wang amesema, China inakaribisha na kuthamini juhudi za Saudi Arabia, Oman na nchi nyingine za eneo hilo katika kutuliza hali ya Yemen na kufikia usitishaji vita wa kudumu, na kuunga mkono pande zinazohusika kufikia suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Yemen kwa njia ya mazungumzo.
Hivi karibuni, Saudi Arabia na Oman zilituma ujumbe kwa pamoja katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a, kufanya mazungumzo na kundi la Houthi, kwa lengo la kumaliza mgogoro huo wa Yemen ambao umedumu kwa miaka mingi.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma