99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais wa Ufaransa: Ulaya yatakiwa kuwa na uwezo wa kujiamulia katika kuchagua wenzi wa ushirikiano

(CRI Online) April 13, 2023

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi ametoa hotuba akisisitiza kuwa Ulaya inatakiwa kudumisha ufunguaji mlango, huku ikilinda mamlaka ya uchumi. Kwa njia hiyo tu, ndiyo inaweza kujichagulia wenzi wa ushirikiano na kuweka hatma yake mikononi mwa watu wa Ulaya.

Amesema, uhuru na kujiamulia ni muhimu kwa Ulaya, bara hilo linatakiwa kudumisha mtindo wake wa kujiendeleza na kutotegemea nchi nyingine.

Anaona kuwa kama Ulaya ikitaka kujihakikishia ushindani, inatakiwa kuimarisha uvumbuzi na mageuzi na kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, ikiwemo kuongeza mafunzo ya kiufundi kwa nguvukazi za nchi mbalimbali barani Ulaya, na kuunganisha soko la Ulaya ili kuvutia mitaji na watu wenye ujuzi. Amesema Ulaya inatakiwa kuendeleza teknolojia ya hali ya juu na kuonya kuwa kutegemea teknolojia za nchi nyingine kutaifanya ikabiliwe na hatari.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha