

Lugha Nyingine
Bahrain na Qatar zaamua kurejesha tena kawaida uhusiano wa kidiplomasia
(CRI Online) April 13, 2023
Bahrain na Qatar zimerejesha tena kawaida uhusiano wa kidiplomasia kati yao, ikiwa ni kuendana na kanuni za usawa wa pande zote na kuheshimu mamlaka na uhuru wa kila nchi, na kudumisha umoja ndani ya Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC).
Wajumbe kutoka nchi hizo mbili wamekutana Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, ambapo pia waliamua kustawisha uhusiano kati ya nchi hizo kwa mujibu wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na masharti ya Mkataba wa Vienna wa Uhusiano wa Kidiplomasia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma