

Lugha Nyingine
Mtaalamu asema Uvujaji wa nyaraka za upelelezi zilizoainishwa kuwa siri kunaonyesha undumila kuwili wa Marekani
Bango kubwa lenye kauli mbiu likionekana mbele ya jengo la Bunge la Marekani wakati wa maandamano dhidi ya ufuatiliaji wa mawasiliano binafsi ya watu unaofanywa serikali huko Washington D.C., Marekani, Oktoba 26, 2013. (Xinhua/Fang Zhe)
ZAGREB - Hrvoje Klasic, profesa katika Chuo Kikuu cha Zagreb cha Croatia amesema Jumatano, kwamba Ripoti za kuvuja kwa nyaraka za upelelezi zilizoainishwa kuwa siri za Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon kunaonyesha undumila kuwili wa Marekani kwani inajishughulisha na ujasusi wa kupeleleza nchi, ikiwa ni pamoja na washirika wake, huku ikishutumu nchi nyingine kujihusisha na ufuatiliaji wa mawasiliano binafsi ya watu mtandaoni.
"Katika mambo mengi, Marekani ina tabia za ndumilakuwili, kwani inawashutumu wengine kwa kile inachofanya yenyewe. Tabia za ndumilakuwili zinaonekana katika nyanja nyingi za siasa za Marekani leo," Profesa Klasic ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.
Uvujaji wa nyaraka hizo zilizoainishwa kuwa siri za Marekani unaonyesha kwamba Washington inajaribu kumpeleleza kila mtu, ikiwa ni pamoja na washirika wake, "kwa sababu ni wazi haimwamini mtu yeyote kabisa," Klasic amesema, huku akiongeza kuwa ni suala sawa na Ukraine, kwani nyaraka zinaonyesha kuwa Marekani imekuwa ikimpeleleza Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Waandamanaji wakiwa wameshikilia mabango kupinga ufuatiliaji wa serikali wa mawasiliano binafsi ya watu huko Washington D.C., Marekani, Oktoba 26, 2013. (Xinhua/Fang Zhe)
Kusikiliza mawasiliano binafsi ya kila mtu, ikiwa ni pamoja na washirika wake, si jambo geni kwa Marekani, na uvujaji wa nyaraka za kijeshi zilizoainishwa kuwa siri kwa hakika "unatoa picha mpya" juu ya usuli wa mgogoro wa Ukraine, Klasic ameeleza.
Picha iliyopigwa Agosti 15, 2022 ikionyesha jengo la makao makuu ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) likiwa nyuma ya uzio wa usalama huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)
Mei 2021, Shirika la Utangazaji la Taifa la Denmark, DR News liliripoti kwamba Idara ya Ujasusi wa Ulinzi ya Denmark ililipa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) ufikiaji wa mtandao wa wazi wa kupeleleza wanasiasa wakuu wa nchi jirani, akiwemo aliyekuwa Chansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Ufichuzi huo ulipunguza uhusiano kati ya Marekani na Ulaya na ulionyesha kuwa Jumuiya ya NATO ilikabiliwa na changamoto nyingi, Klasic amesema.
Picha iliyopigwa Tarehe 8 Desemba 2022 ikionyesha jengo Bunge la Marekani, Capitol huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma