99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Tanzania kuweka WIFI kwenye maeneo ya umma ili kuhimiza matumizi ya ICT

(CRI Online) April 12, 2023

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Bw. Mathew Kundo amesema Tanzania inapanga kuweka mtandao wa intaneti isiyotumia nyaya (WIFI) kwenye maeneo ya umma ili kuhimiza matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya habari.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa Bunge unaoendelea nchini humo, Bw. Kundo amesema serikali ya Tanzania inawekeza katika habari za kidigitali ili kuunga mkono maendeleo ya uchumi.

Pia amesema, serikali imetambua kuwa ni lazima kutoa huduma ya wazi ya WIFI, ili raia waweze kushiriki kwenye masuala ya jamii na uchumi, hatua itakayosaidia kuhimiza maendeleo na biashara.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha