99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Utafiti waonesha zaidi ya nusu ya watu wazima nchini Marekani wamekumbana na tukio linalohusika na ukatili wa bunduki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2023

https://english.news.cn/20230412/f78f563f4f2b43ef99347d810a12bae0/20230412f78f563f4f2b43ef99347d810a12bae0_54f19a6e-9375-4a75-a739-a7ceeba601f7.jpg

Watu wakikusanyika kwenye maandamano ya kulaani kuongezeka kwa ukatili wa kutumia bunduki huku wakiwataka wanasiasa kuchukua hatua huko Washington, D.C., Marekani, Juni 11, 2022. (Xinhua/Liu Jie)

LOS ANGELES – Matokeo yaliyotolewa Jumanne ya utafiti mpya yameonesha kuwa, zaidi ya nusu ya watu wazima nchini Marekani wamekumbana na tukio linalohusika na ukatili wa kutumia bunduki.

Utafiti huo mpya kutoka kwa Mfuko wa Familia ya Kaiser, shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu California, Marekani unaonyesha kuwa asilimia 54 ya watu wazima nchini Marekani wao binafsi au wanafamilia wao ambao wameathiriwa na tukio linalohusika na bunduki, kama vile kushuhudia ufyatuaji risasi, kutishiwa kwa bunduki, au kujeruhiwa au kuuawa kwa bunduki.

Walipoulizwa kuhusu uzoefu wao binafsi, mmoja kati ya watano (idadi inayowakilisha asilimia 21 ya watu wazima wa Marekani) waliripoti kwamba wametishiwa kwa bunduki, huku karibu wengi wao (asilimia 17) wakisema wameshuhudia mtu akipigwa risasi.

Walipoulizwa kuhusu wanafamilia wao, takriban watu wazima watatu kati ya kumi (asilimia 31) wamesema wanafamilia wao wametishiwa kupigwa risasi, huku sehemu kama hiyo (asilimia 28) ikisema kuwa mwanafamilia mmoja ameshuhudia mtu akipigwa risasi. Mmoja kati ya watu wazima watano (asilimia 20) amesema mwanafamilia amejeruhiwa kwa bunduki, na asilimia 19 wanasema mwanafamilia mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi, ikiwa ni pamoja na vifo vya kujifyatulia risasi, kwa mujibu wa utafiti huo.

Utafiti huo umebaini kuwa watu wazima watatu kati ya wanne katika kaya zilizo na bunduki wanasema angalau bunduki moja nyumbani kwao ama haijafungwa, imeandaliwa kufyatua risasi, au kuhifadhiwa ikiwa na risasi.

Utafiti huo umebaini kuwa majeraha na vifo vinavyohusika na bunduki, pamoja na wasiwasi kuhusu ukatili wa kutumia bunduki, huathiri kwa njia isiyo sawa watu wa rangi nchini Marekani hususan jamii ya Wamarekani wenye asili ya Afrika na Wahispania.

https://english.news.cn/20230412/f78f563f4f2b43ef99347d810a12bae0/20230412f78f563f4f2b43ef99347d810a12bae0_b3dafda1-aed1-42cb-980e-0967ca226b5f.jpg

Watu wakifanya maandamano ya kulaani kuongezeka kwa ukatili wa kutumia bunduki huku wakiwataka wanasiasa kuchukua hatua huko Washington, D.C., Marekani, Juni 11, 2022. (Xinhua/Liu Jie)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha