

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akikutana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa na Kujenga Amani Rosemary A. DiCarlo mjini Beijing, China, Aprili 11, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang Jumanne amekutana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa na Kujenga Amani Rosemary A. DiCarlo mjini Beijing.
Qin amesema, ikiwa kwa matumaini ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, China imeshiriki kwa ukamilifu kazi za Umoja wa Mataifa, kutekeleza kwa uthabiti wajibu wake wa kimataifa, kutetea kikamilifu mshikamano na ushirikiano, na kutoa bidhaa za umma kwa Dunia.
"China itaunga mkono kithabiti Umoja wa Mataifa katika kubeba jukumu la kiujenzi katika kusukuma mbele masuala ya kimataifa na kikanda, na iko tayari kuwa mshirika wa kuaminika na wa kutegemewa wa Umoja wa Mataifa katika kudumisha amani ya Dunia na kukuza maendeleo kwa pamoja," Qin amesema.
Kwa upande wake, DiCarlo ameeleza matumaini yake kuwa Umoja wa Mataifa utaimarisha ushirikiano na China na kupendekeza kwa pamoja masuluhisho zaidi kwa masuala muhimu ya kimataifa na kikanda.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma