99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uvujaji wa nyaraka za upelelezi unafichua ujasusi wa Marekani dhidi ya nchi maadui na washirika: Washington Post

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2023

Picha iliyopigwa Februari 19, 2020 ikionyesha Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon yakionekana kutoka kwenye ndege juu ya Washington D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Picha iliyopigwa Februari 19, 2020 ikionyesha Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon yakionekana kutoka kwenye ndege juu ya Washington D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

NEW YORK - Mwishoni mwa wiki, wakati maofisa wa Marekani na washirika wake wa nchi mbalimbali walipokuwa wakihangaika kuelewa jinsi nyaraka nyingi za siri za upelelezi zilivyoonekana kwenye mtandao wa intaneti, walipigwa na butwaa, na mara kwa mara kukasirishwa, kwa kiwango cha undani wa ajabu wa namna faili hizo zilivyofichua kuhusu jinsi Marekani inavyopeleleza nchi marafiki na maadui vile vile, limeripoti Gazeti la Washington Post Jumamosi.

"Nyaraka hizo, ambazo zinaonekana kuwa, sehemu zake fulani zimetoka kutoka Pentagon na zimeainishwa kama nyaraka za siri, zinatoa habari kuhusu mbinu za vita vya Ukraine, pamoja na uwezo wa kupambana wa nchi hiyo," imesema ripoti hiyo.

Nyaraka nyingi zinaonekana kuwa zimetayarishwa wakati wa majira ya baridi kwa ajili ya maofisa wakuu wa kijeshi, lakini pia zilitolewa kwa wafanyakazi wengine wa Marekani na wafanyakazi wa kandarasi wakiwa na vibali vinavyohitajika vya usalama, ripoti hiyo imesema, ikimnukuu ofisa mmoja wa ulinzi.

Nyaraka zingine ni pamoja na uchanganuzi kutoka kwa mashirika ya upelelezi ya Marekani kuhusu Russia na nchi nyingine kadhaa, zote zikiangazia habari zilizokusanywa kutoka kwa vyanzo vya siri, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

"Mfululizo wa maelezo na muhtasari unafungua dirisha nadra juu ya utendaji wa ndani wa ujasusi wa Marekani," ripoti hiyo imesema.

Miongoni mwa siri nyingine, zinaonekana kufichua mahali ambapo CIA imeajiri mawakala wa kibinadamu kwa siri kufuatilia mazungumzo ya siri ya viongozi wa Dunia; sauti inayoonyesha mamluki wa Russia walijaribu kupata silaha kutoka kwa nchi mshirika wa NATO ili kuzitumia dhidi ya Ukraine; na ni aina gani ya picha za setilaiti ambazo Marekani hutumia kufuatilia majeshi ya Russia, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya hali ya juu ambayo inaonekana kwa shida sana, na ni vigumu kutambuliwa hadharani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha