

Lugha Nyingine
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China asema China siyo chanzo cha "mtego wa madeni" kwa Nchi za Afrika
BEIJING - China siyo chanzo cha "mtego wa madeni" wa nchi za Afrika, bali ni mshirika wa kuzisaidia nchi hizo na nchi nyingine zinazoendelea kuepuka "mtego wa umaskini", Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema Jumatatu.
Wang ametoa kauli hiyo wakati akijibu shutuma zinazotolewa dhidi ya China na baadhi ya maofisa waandamizi wa Marekani na maofisa wa Benki ya Dunia kuhusiana na suala la deni la Afrika.
"Tuhuma hizo hazina msingi wowote," Wang amesema. "China inalipa umuhimu mkubwa suala la deni la Afrika na kusaidia nchi za Afrika kukabiliana nalo. China imechangia zaidi Mpango wa Kusimamisha Huduma ya Madeni (DSSI) kuliko nchi nyingine yoyote mwanachama wa Kundi la 20 (G20)."
Amesema, kwa mujibu wa utafiti wa hivi punde wa Programu ya Utafiti wa China na Afrika katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, China imechangia asilimia 63 ya kusimamishwa kwa huduma ya madeni chini ya DSSI. Utafiti huo umebainisha kuwa China imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kuwasiliana na pande nyingine zinazoshiriki, na imetekeleza wajibu wake katika kutekeleza kwa ufanisi DSSI.
Wang amemnukuu Makamu wa Rais wa Nigeria Yemi Osinbajo akielezea wasiwasi wa serikali za Magharibi juu ya kile kinachojulikana kama "mtego wa madeni wa China" kama wa kukuza hali ya mambo kuliko uhalisia.
Osinbajo alisema, nchi za Afrika hazina haja ya msamaha kuhusu uhusiano wao wa karibu na China. Afrika inahitaji mikopo na miundombinu. China inajitokeza wapi na lini nchi za Magharibi hazitafanya au zinasitasita.
"Ujanja wao umedhalilishwa na sasa wanapata ugumu zaidi kupata uungwaji mkono katika nchi zinazoendelea na jumuiya kubwa ya kimataifa," Wang amesema.
Amesema, kwa mujibu wa Takwimu za Madeni ya Kimataifa za Benki ya Dunia, taasisi za fedha za kimataifa na wakopeshaji wa kibiashara wanashikilia karibu robo tatu ya jumla ya deni la nje la Afrika. Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zinachangia karibu asilimia 70 ya jumla ya deni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma