99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Gazeti la Financial Times: Kuizingira China si mkakati wa kudumu unaofaa

(CRI Online) April 07, 2023

Gazeti la Financial Times la Uingereza limechapisha makala iliyoandikwa na Edward Luce akisema, China iko sahihi kwa kuona kwamba Marekani ndio inaizuia, kuizingira na kuishinikiza, lakini ameonya kuwa kufanya hivyo si mkakati wa kudumu unaofaa.

Mwandishi huyu raia wa Marekani amesema sababu kadhaa zinazopelekea hali ya wasiwasi ya uhusiano kati ya China na Marekani ni kwamba Marekani haitaki kuacha nafasi yake ya kipekee inayofuatiliwa na nchi nyingine.

Anaeleza kuwa, jaribio la Rais Joe Biden kutaka kushirikiana na China liligonga mwamba baada ya Marekani kudungua puto la kuchunguza hali ya hewa la China. Amesema kwamba hatua kama hiyo ya kupita kiasi ilichochewa na makubaliano ya vyama viwili vya Democrats na Republican ambavyo vinachukulia mawasiliano yoyote na China kama ni udhaifu.

Amesisitiza kuwa Wamarekani wengi wanaona kuwa Marekani na China ziko katika vita baridi, lakini Marekani haiwezi kupata njia ya kushinda, kwa kuwa kuifanya China iweze kuitii si mkakati.

Amesema nchi inayojiamini kwa nguvu zake haipaswi kuogopa mazungumzo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha