

Lugha Nyingine
Trump ashtakiwa kwa makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara, mwenyewe akana mashtaka
Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameshtakiwa kwa makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara zake, na kufikishwa katika Mahakama ya makosa ya Jinai ya Manhattan Jijini New York, na kuwa rais wa kwanza mstaafu wa Marekani kushtakiwa kwa makosa ya jinai.
Mwanasheria wa Wilaya ya Manhattan Bw. Alvin Bragg alitangaza mashtaka hayo baada ya Bw. Trump kufikishwa mahakamani, akimtuhumu kwa kughushi rekodi za biashara zake katika Mji wa New York, ili kuwaficha wapiga kura wa Marekani taarifa za matendo yake maovu na shughuli zisizo halali kabla na baada ya uchaguzi wa 2016.
Bw. Bragg amesema wakati wa uchaguzi, Bw. Trump na wenzake wengine walitumia mpango wa "kamata na kuua" ili kutambua, kununua, na kuficha habari mbaya kumhusu yeye na kuongeza matarajio yake ya uchaguzi.
Bw. Trump amekanusha mashtaka na kusema kuwa uchunguzi wa uhalifu unaoongozwa na Bw. Bragg, ambaye ni mwanachama wa Democrat, unachochewa kisiasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma