

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Yoshimasa Hayashi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani, mjini Beijing, China, Aprili 2, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Yoshimasa Hayashi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani, mjini Beijing siku ya Jumapili.
Huku akieleza kuwa China na Japan ni majirani wa karibu na nchi muhimu za Asia, Waziri Mkuu Li amesema kudumisha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Japan kunanufaisha siyo tu maslahi ya kimsingi ya watu wa pande hizo mbili, bali pia amani, utulivu na ustawi wa kikanda.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 45 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Amani na Urafiki kati ya China na Japan.
Waziri Mkuu Li ametoa wito kwa pande hizo mbili kudurusu na kufuata vipengele vya mkataba huo ili kuendeleza kithabiti uhusiano wa kudumu kati ya China na Japan unaojumuisha amani na urafiki.
Waziri Mkuu Li amesisitiza kwamba masuala makuu ya kanuni, kama vile historia na suala la Taiwan, ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Japan, ambayo yanataka masuluhisho ya dhati, ya upole na makini.
Ameeleza matumaini yake kuwa pande hizo mbili zitalinda kwa pamoja biashara huria, kutumia ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kuendeleza kikamilifu mchakato wa mafungamano ya kikanda, kudumisha utulivu na mtiririko mzuri wa minyororo ya viwanda, na kuchangia maendeleo ya kikanda na kimataifa.
Kwa upande wake Hayashi pamoja na kueleza kuwa Japan iko tayari kushirikiana na China kuadhimisha miaka 45 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Amani na Urafiki kati ya China na Japan kama fursa ya kudumisha uhusiano, amesema kuwa, Japan na China zina uwezo mkubwa wa ushirikiano katika maeneo mbalimbali, na kuongeza kuwa Japan imejitolea kukuza ushirikiano wake na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma