

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahimiza kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi wa aina zote
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumanne ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kukabiliana na ubaguzi wa rangi popote pale unapotokea, na kukomesha aina zote za ubaguzi wa rangi.
Guterres ametoa wito huo alipokuwa akihutubia katika hafla ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi ambayo inaadhimishwa Tarehe 21, Machi kila Mwaka.
“Ubaguzi wa rangi ni moja ya nguvu haribifu zinazogawa jamii, zinazohusika na vifo na mateso kwa kiwango cha kutisha katika historia,” amesema Guterres.
Ameongeza kuwa, leo hii, ubaguzi wa rangi na urithi wa utumwa na ukoloni vinaendelea kuharibu maisha, kuzitenga jamii na kupunguza fursa, kuzuia mabilioni ya watu kufikia uwezo wao kamili.
"Chuki dhidi ya raia wageni katika nchi nyingine, mashambulizi na kauli zenye kubeba chuki vinaongezeka. Viongozi wa kisiasa wanawatoa kafara wahamiaji, kwa athari mbaya," amesema Guterres.
"Lazima tuchukue hatua kukabiliana na ubaguzi wa rangi popote pale unapotokea, ikiwa ni pamoja na kupitia njia za kisheria."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma