

Lugha Nyingine
Wizara ya Mambo ya Nje ya China yatoa ripoti kuhusu hali ya demokrasia nchini Marekani Mwaka 2022
BEIJING - Wizara ya Mambo ya Nje ya China Jumatatu imetoa ripoti kwenye tovuti yake yenye kichwa kinachosomeka "Hali ya Demokrasia nchini Marekani: 2022."
Kwa kuzingatia ukweli, maoni ya vyombo vya habari na maoni ya wataalamu, ripoti hiyo inalenga kuwasilisha picha halisi ya demokrasia ya Marekani katika mwaka uliopita.
Ripoti hiyo inabainisha kwamba demokrasia ya Marekani ilikuwa katika machafuko nchini humo na kwamba njia ya uharibifu na maafa yaliachwa nyuma wakati Marekani ikiingilia kati na kulazimisha demokrasia yake duniani kote. Inatarajiwa kwamba ripoti hiyo itasaidia kuonesha sura halisi ya demokrasia ya Marekani kwa watu wengi zaidi duniani kote.
Mbali na utangulizi na hitimisho, ripoti hiyo ina sehemu mbili zenye sura mbili za "Demokrasia ya Marekani katika magonjwa ya kudumu" na "Ulazimishaji wa Marekani wa 'demokrasia' umesababisha machafuko duniani kote."
“Mwaka 2022, mzunguko mbaya wa majigambo ya kidemokrasia, siasa duni na jamii iliyogawanyika viliendelea nchini Marekani,” ripoti hiyo inasema, na kuongeza kuwa matatizo kama vile siasa za pesa, siasa za utambulisho, mipasuko ya kijamii, na pengo kati ya matajiri na maskini yalizidi kuwa mabaya.
Ripoti hiyo inasema kuwa, maradhi yanayoikumba demokrasia ya Marekani yameambukiza sana seli za siasa na jamii za Marekani, na kufichua zaidi kushindwa kwa utawala wa Marekani na kasoro za kitaasisi.
“Hata hivyo, Marekani inakataa kukiri matatizo mengi na migogoro ya kitaasisi inayokabili demokrasia yake nchini kwake na kwa ukaidi inadai kuwa kielelezo na kinara wa demokrasia kwa Dunia” ripoti hiyo inasema huku ikiitaka Marekani kuacha kuchochea migawanyiko kwa kisingizio cha demokrasia na kuzilamisha nchi kuchukua upande.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma