99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wazimamoto waitwa mashujaa kwa kuokoa watu waliokwama kwenye theluji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2023

(Picha inatoka ChinaDaily.)

Hivi karibuni, askari wa kikosi cha zimamoto cha Mji wa Hulunbuir wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani walifaulu kuokoa watu wanane waliokwama kwenye theluji kubwa. Habari iliyoripotiwa Jumanne na televisheni ya China CCTV ilisema, picha za wazimamoto hao zilipata umaarufu sana kwenye mtandao wa intaneti wa China, zikigusa mioyo ya watu wengi.

“Mhusika mkuu katika picha maarufu ya 'mtu aliyeganda' ni Ge Zebing, ambaye ana umri wa miaka 26 na amekuwa akifanya kazi ya zimamoto kwa miaka tisa sasa.

Tarehe 10, Machi, hali ya hewa imebadilika kuwa ya baridi kali kwa ghafla huko Hulunbuir, huku kukiwa na kimbunga cha upepo cha daraja la saba na theluji kubwa. Saa 6:46 mchana siku hiyo, kikosi cha uokoaji ambacho Ge ni sehemu yake kilipokea simu ya kuomba msaada, ikisema kulikuwa na madereva waliokuwa wamekwama kwenye barabara ya kitaifa ya 332 katika eneo la Hailaar.

Saa 8:18 mchana, waokoaji wa kikosi hicho walifika kwenye sehemu hiyo, na kukuta theluji ikiwa nzito sana yenye upenyo wa karibu mita moja.

“Upepo wa siku hiyo ulikuwa mkali sana, na theluji ilipopiga uso wangu iliuma sana kama kuchomwa sindano. Halijoto ya hewa ilihisiwa kuwa chini ya nyuzi 20 chini ya sifuri, na barafu liliganda kwenye miili yetu sote” amesema Ge.

Baada ya kutekeleza uokoaji kwa zaidi ya saa moja, watu wote wanane waliokwama kwenye magari matatu waliokolewa.

Ge anasema, wakati akitekeleza uokoaji, alichofikiri ni kuwaokoa tu kutoka kwenye hatari watu waliokuwa wamekwama kwa haraka kadri iwezekanavyo. Alikuwa hajahisi baridi na uchovu aliokuwa nao hadi baada ya uokoaji kukamilika.

“Nimefurahi sana na kuridhika kwamba nilikamilisha jukumu langu” amesema.

Wazimamoto hao wamesifiwa na watumiaji wa mtandao wa intaneti wa China kuwa “mashujaa wazuri zaidi”. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha