99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China kwa mara nyingine tena yaitaka Marekani kuacha mara moja ghiliba za kisiasa juu ya kufuatilia chanzo cha UVIKO

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2023

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema Alhamisi kwamba, China kwa mara nyingine inautaka upande wa Marekani kuacha mara moja ghiliba za kisiasa juu ya ufuatiliaji wa chanzo cha UVIKO, kushiriki kwa hiari na WHO data za maambukizi ya mapema nchini Marekani yanayoshukiwa.

Msemaji Mao aliyasema hayo baada ya Baraza la Juu la Bunge la Marekani kupitisha Sheria ya Chanzo cha UVIKO-19 ya Mwaka 2023 siku chache zilizopita, ambayo inasema kwamba janga la UVIKO-19 linaweza kuwa lilianzia China. Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi ya Marekani Avril Haines Jumatano alieleza kuwa hakuna makubaliano ya pamoja kati ya mashirika ya kijasusi ya Marekani kuhusu mlipuko huo ni matokeo ya kuvuja kwa vitusi kutoka maabara au kuibuka kiasili kutokana na kugusana na mnyama aliyeambukizwa. Ukiacha hili, mtaalamu wa virusi wa Poland Agnieszka Szuster-Ciesielska hivi majuzi alisema katika mahojiano kwamba nadharia ya "virusi vya Korona kuvuja maabara" iliyotangazwa upya na Wizara ya Nishati ya Marekani na Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI ni ya kutafuta hali ya kutimua vumbi, na haina msingi wa kweli au wa kisayansi.

Msemaji huyo amesema, Kwa muda sasa, Marekani imekuwa ikitumia kufuatilia kisiasa chanzo cha UVIKO, na kama silaha na mkakati kwa miezi mingi, imeruhusu suala la sayansi kutawaliwa na watunga sheria na mashirika ya ujasusi na kueneza simulizi kama vile nadharia ya "kuvuja maabara" bila ushahidi wowote ili kuichafua na kuishambulia China.

"Hii imetia sumu kali kwenye anga hali ya ufuatiliaji duniani wa chanzo cha UVIKO unaofanyika kwenye msingi wa sayansi , na hali hii imehisiwa na watu duniani kote," amesema.

Akidhihirisha kuwa, msimamo wa China ni wa kithabiti juu ya ufuatiliaji wa chanzo cha UVIKO-19, China imeunga mkono na kushiriki katika ufuatiliaji wa chanzo unaotegemea sayansi duniani tangu siku ya kwanza.

"Wakati huo huo, tumekuwa tukipinga vikali aina zote za ghiliba za kisiasa juu ya suala hili," Mao amesema, na kuongeza kuwa, ghiliba za kisiasa zinazofanywa na Marekani ndiyo kikwazo kikuu kwa utafiti unaotegemea sayansi juu ya chanzo cha UVIKO.

Huku akisema kuwa Marekani haijafanya chochote kuwajibika katika kutafuta chanzo, haijawahi kuvialika vikundi vya wataalam wa WHO nchini Marekani kwa ajili ya kufanya utafiti wa pamoja, au kutoa data zozote za mapema juu ya chanzo cha COVID na imeziba masikio kwenye maswala yanayofuatiliwa na Dunia kuhusu kambi za kijeshi za kibiolojia za Marekani huko Fort Detrick na kote duniani.

"Kwa mara nyingine tena tunautaka upande wa Marekani uache mara moja ghiliba za kisiasa juu ya suala hili, kujibu ufuatiliaji halali wa Dunia, kushiriki kwa hiari na WHO katika data za maambikizi ya mapema yanayoshukiwa nchini Mareakni, kufichua habari kuhusu maabara yake ya kibaolojia huko Fort Detrick na kote duniani, na kuipa Dunia nzima ukweli unaostahili," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha