

Lugha Nyingine
WMO latoa idhini kwa mpango wa usimamizi wa hewa ukaa duniani
(CRI Online) Machi 08, 2023
Baraza tendaji la Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) jana lilipitisha mpango mpya wa miundombinu ya usimamizi juu ya hewa ukaa duniani, ili kutoa zaidi taarifa muhimu na kuunga mkono kuchukua hatua katika kupunguza utoaji wa hewa ukaa.
Shirika hilo limesema kwa sasa shughuli nyingi za kimataifa na za nchi zinazohusiana na hewa ukaa zinaungwa mkono na sekta ya utafiti. Kwa sasa hakuna mawasiliano kamili ya kimataifa juu ya usimamizi wa hewa ukaa ardhini na angani.
WMO itafanya juhudi za uratibu chini ya mfumo wa ushirikiano wa kimataifa, na kutoa mchango kadri iwezekanavyo kuhusu usimamizi wa hewa ukaa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma