99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Watu 9 wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Kusini Magharibi mwa Pakistan

(CRI Online) Machi 07, 2023

Polisi wa Pakistan walisema, watu 9 wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea jana mkoani Balochistan, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Polisi wamesema, mshambuliaji alipanda pikipiki iliyotegwa mabomu na kugonga lori lililobeba askari 22. Mpaka sasa hakuna kundi lolote au watu binafsi waliokiri kuhusika na shambulizi hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha