99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais wa Iran aitaka IAEA kuchukua mtazamo wa "kitaalamu" katika suala la nyuklia la Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2023

Rais wa Iran Ebrahim Raisi (Kulia) akikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi mjini Tehran, Iran, Machi 4, 2023. (Tovuti ya Ikulu ya Iran/ Xinhua)

TEHRAN - Rais wa Iran Ebrahim Raisi Jumamosi amesema kwamba, anatumai Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) linaweza kuchukua mtazamo wa "kitaalamu" katika suala la nyuklia la Iran na kuzuia baadhi ya nchi kuathiri maamuzi ya shirika hilo la nyuklia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Ikulu ya Iran Raisi ameyasema hayo kwenye mkutano wake na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi aliyetembelea mji mkuu Tehran.

Nchi kama Israel na Marekani zinatumia suala la nyuklia kama "kisingizio" cha kuwashinikiza zaidi watu wa Iran, amesema rais huyo, akiashiria kuwa ni Marekani iliyokiuka makubaliano ya nyuklia ya Mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani.

“Iran imekuwa na kiwango cha juu zaidi cha ushirikiano na IAEA, inatarajia shirika hilo kusema ukweli kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran pamoja na ahadi ya nchi katika kanuni zake,” ameeleza.

Wakati huo huo, mkuu huyo wa IAEA amefurahia kuitembelea Iran na kukutana na rais wa nchi hiyo, akisema timu ya IAEA inayoongozwa na yeye mwenyewe imekuwa na mikutano "ya kiujenzi na hamasa " na upande wa Iran.

Grossi aliwasili Tehran siku ya Ijumaa kwa ziara ya siku mbili, ambapo pia alifanya mazungumzo na Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian.

Katika miezi ya hivi karibuni, IAEA imekuwa ikiikosoa Iran kwa kutokulipa ushirikiano shirika hilo.

Mwezi Novemba 2020, Bodi ya Wakurugenzi ya IAEA ilipitisha azimio lililopendekezwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambalo liliitaka Iran kushirikiana na wachunguzi wa shirika hilo kuhusu madai ya "mabaki ya uranium" katika baadhi ya maeneo yake ambayo "hayajatangazwa wazi".

Iran imekuwa ikikanusha mara kwa mara madai hayo na kusisitiza matumizi ya amani ya mpango wake wa nyuklia. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian (wa pili kushoto) akikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi (wa pili kulia) mjini Tehran, Iran, Machi 4, 2023. (Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha