

Lugha Nyingine
China Bara yapinga vikali Marekani kuiuzia silaha Taiwan
BEIJING - Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, Ma Xiaoguang siku ya Alhamisi amesema, China inapinga vikali hatua ya Marekani kuiuzia silaha Taiwan ambayo ni eneo la China.
“Hatua hiyo ya Marekani inakiuka vibaya kanuni ya kuwepo kwa China moja na zile taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, hususan Taarifa ya Agosti 17,” amesema Ma, wakati akijibu swali kutoka kwa wanahabari kuhusu uamuzi wa Marekani kuiuzia silaha Taiwan.
Ma ameongeza kuwa, hatua hiyo inaunga mkono makundi ya wanaotaka kuifanya “Taiwan ijitenge” na inaharibu amani na utulivu kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan.
"Tunaitaka Marekani kutii kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na kusitisha uuzaji wa silaha na mawasiliano ya kijeshi na Taiwan," Ma amesema.
Ma pia ameonya uongozi wa Chama cha Kidemokrasia cha Taiwan kwamba jaribio lolote la kutumia nguvu kupinga muungano wa taifa au kushirikiana na nguvu ya nje kuifanya “Taiwan ijitenge " halitafanikiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma