99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ahimiza ushirikiano wenye nguvu zaidi wa G20 ili kukuza ushirikiano wa pande nyingi na maendeleo ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akihudhuria kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kundi la 20 (G20) mjini New Delhi, India, Machi 2, 2023. (Picha na Javed Dar/Xinhua)

NEW DelHI - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang Alhamisi ametoa wito kwa nchi wanachama wa Kundi la 20 (G20) kufanya ushirikiano wa karibu zaidi katika kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi na kukuza maendeleo ya kimataifa.

Qin ametoa wito huo alipokuwa akihutubia kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa G20 hapa Alhamisi.

Kwenye hotuba yake hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa China amezitaka nchi wanachama wa G20 kujitolea kwa ushirikiano wa pande nyingi, kujenga maelewano na utandawazi, na kutekeleza makubaliano na kutoa matokeo ya Mkutano wa G20 wa Bali uliofanyika Novemba 2022.

Qin amesema, kwa kukabiliwa na hali ya msukosuko wa kimataifa na kuongezeka kwa changamoto za kimataifa, nchi za G20 lazima ziimarishe ushirikiano na kutoa mchango wake katika maendeleo na ustawi wa Dunia.

“Nchi wanachama wa G20 zinahitaji kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kutilia maanani mfumo wa kimataifa unaoshikilia Umoja wa Mataifa na utaratibu wa kimataifa unaofuata sheria za kimataifa, na kufuata kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa zinazoungwa mkono na nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa” amesema.

"Hakuna yeyote anayepaswa kujihusisha na siasa za madaraka au hata mapambano ya kambi," ameeleza Qin.

Amesema nchi wanachama wa G20 zinapaswa kukuza maendeleo ya utandawazi, kukataa msimamo wa upande mmoja na kujihami kiuchumi, na kuhakikisha uendeshaji mzuri wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi.

Ametoa mwito wa kufanyika kwa juhudi za kuyafanya maendeleo ya kimataifa kuwa "jumuishi zaidi, yenye uhimilivu na yenye manufaa kwa wote," akiongeza kuwa Mpango wa Maendeleo ya Dunia unaopendekezwa na China umetoa chaguo jipya la kuongeza utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa .

Ili kutekeleza vizuri maamuzi ya Mkutano wa Bali, Qin ametoa wito wa kuimarisha uratibu wa sera za uchumi mkuu, kulinda usalama wa chakula na nishati, kuboresha uongozi wa kiuchumi duniani na kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo wa kimataifa.

"China imesitisha malipo ya deni kwa mara nyingi zaidi kuliko nchi mwanachama mwingine yeyote wa G20, na kushiriki katika mpango wa kushughulikia deni chini ya Mfumo wa Pamoja," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha