99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China Wang Yi akutana na ujumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 02, 2023

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na ujumbe unaoongozwa na Romenio Pereira, Katibu wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazili hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 1, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC amekutana na ujumbe ulioongozwa na Romenio Pereira, Katibu wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil mjini Beijing siku ya Jumatano.

Kwenye mazungumzo kati yao Wang Yi amesema kwamba China na Brazil zote ni nchi kubwa zinazoendelea zenye mchango wa kimataifa na nchi zenye masoko yanayoibuka. Amesema China daima inautendea uhusiano wa nchi hizo mbili kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na nchi hizo mbili zina ushirikiano wenye manufaa katika sekta mbalimbali na uratibu wa karibu katika masuala ya kimataifa.

Huku akieleza kuwa uhusiano kati ya China na Brazil unahusiana na maendeleo ya nchi hizo mbili pamoja na amani na utulivu duniani, Wang amesema CPC kiko tayari kuwa na mabadilishano ya kina ya uzoefu wa utawala wa nchi na Chama cha Wafanyakazi cha Brazil na kufungua mustakabali mpya wa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Brazil.

Kwa upande wake Pereira amesema kuwa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil kinatilia maanani sana kuimarisha mabadilishano ya uzoefu na CPC kuhusu uongozi wa chama na utawala wa nchi, na kinatarajia kusukuma mbele ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya watu wa nchi hizo mbili.

Liu Jianchao, Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC pia alikutana na ujumbe wa Pereira siku ya Jumatano. Pande hizo mbili zimebadilishana maoni kwa kina kuhusu kuimarisha urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili, kuimarisha hali ya kufundishana kuhusu uongozi wa chama na utawala wa nchi , na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Brazil.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha