99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Ufumbuzi unaotolewa na Afrika ni muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu

(CRI Online) Machi 02, 2023

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed ameutaja ufumbuzi unaotolewa na Afrika kama ni jambo la muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) katika Afrika.

Bi Amina amesema hayo wakati akihutubia Mkutano wa Tisa wa Baraza la Afrika la Maendeleo Endelevu (ARFSD-9), ambao ulianza Februari 28 na utamalizika leo Machi 2 huko Niamey, Niger.

Bi Amina pia ametoa wito wa kuwepo na uongozi mkubwa zaidi, dhamira na uwekezaji katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Afrika. Pia amewataka viongozi duniani kuwa na matamanio ya wazi ya kupunguza umasikini na kuondoa hali ya kutokuwa na usawa ifikapo Mwaka 2030, na ni lazima wafanye hivi kwa kuwekeza barani Afrika, kwenye uchumi na kwa watu hasa wanawake na vijana.

Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Kuongeza ufufuaji jumuishi na wa kijani kutokana na misukosuko mingi na kufungamanisha na kutekeleza kikamlifu Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika” unaandaliwa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uchumi wa Afrika (UNECA) ikishirikiana na serikali ya Niger pamoja na vyombo vingine.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha