99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mgombea wa chama tawala Tinubu ashinda uchaguzi wa rais Nigeria

(CRI Online) Machi 02, 2023
Mgombea wa chama tawala Tinubu ashinda uchaguzi wa rais Nigeria

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imemtangaza Bola Tinubu kutoka chama tawala cha All Progressives Congress nchini Nigeria kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa Bw. Mahmood Yakubu amesema kuwa Tinubu amepata jumla ya kura milioni 8.79 ambazo ni idadi kubwa zaidi ya jumla ya idadi ya kura zote zilizopigwa wakati wa uchaguzi.

Uchaguzi huo umeelezwa kuwa moja ya uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi katika historia ya nchi hiyo. Rais huyo mteule mwenye umri wa miaka 70 alimshinda mpinzani wake wa karibu, Makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar, ambaye ni mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party aliyepata kura zaidi ya milioni 6.98, akifuatiwa na Peter Obi wa chama cha Labor aliyepata kura takriban milioni 6.1.

Tinubu ambaye aliwahi kuwa gavana na seneta wa Jimbo la Lagos, alikuwa na nia ya kuwa rais kwa miaka mingi ambapo alijenga muundo thabiti wa kisiasa wenye mtandao mkubwa wa wafuasi nchini kote.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha