

Lugha Nyingine
Russia yasitisha rasmi kushiriki kwenye mkataba wa Silaha za Nyuklia na Marekani wa New START
![]() |
Katika picha hii iliyopigwa kutoka kwenye video iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Russia, kombora la masafa marefu la Sarmat linaonekana likifytatuka kwenda angani wakati wa jaribio la urushaji kutoka eneo la Plesetsk, Kaskazini-Magharibi mwa Russia, Machi 30, 2018. |
MOSCOW- Rais wa Russia Vladimir Putin Jumanne ametia saini sheria ya kusimamisha rasmi ushiriki wa Russia kwenye mkataba wake na Marekani wa kupunguza silaha za nyuklia wa New START.
Sheria hiyo iliyotangazwa imesema, sheria inaanza kutumika mara moja, na uamuzi wa kurejesha ushiriki wa Russia katika mkataba huo ni wa mkuu wa nchi .
Katika hotuba yake ya kila mwaka kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaifa Februari 21, Putin alisema Russia ilikuwa na mpango wa kusimamisha ushiriki wake, badala ya kujiondoa kwenye mkataba wa New START. Pia alitaja uwezekano wa mashambulizi ya pamoja ya NATO kwani Uingereza na Ufaransa nazo pia zina silaha za nyuklia ambazo zinatishia Russia.
Siku moja baadaye, mswada wa kusitishwa kwa Mkataba New START ulipitishwa kwa kauli moja na Bunge la Russia na kisha kuwasilishwa kwa Putin ili kuidhinishwa na kuwa sheria rasmi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma