

Lugha Nyingine
Iraq na Iran zajadili hali ya mpaka, ushirikiano wa nchi mbili na usalama wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hussein (Kulia) na mwenzake wa Iran Hossein Amir-Abdollahian wakifanya mkutano wa pamoja na wanahabari mjini Baghdad, Iraq, Februari 22, 2023. (Xinhua/Khalil Dawood)
BAGHDAD - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayezuru Hossein Amir-Abdollahian amefanya mikutano na viongozi wa Iraq siku ya Jumatano huko Baghdad kuhusu hali ya mpaka, ushirikiano wa nchi mbili na usalama wa kikanda.
Kwenye mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hussein alisema kwamba pande hizo mbili zimejadili masuala ya maslahi ya pamoja, ikiwa ni pamoja na hali ya mpaka, na Serikali ya Iraq imechukua hatua za kulinda mpaka wake na Iran dhidi ya kutumika kufanya mashambulizi dhidi ya nchi jirani.
"Katiba ya Iraq inakataza matumizi ya ardhi ya Iraq katika kushambulia nchi jirani," amewaambia waandishi wa habari.
Kwa upande wake, Amir-Abdollahian amewaambia waandishi wa habari kwamba Iran inaunga mkono kuimarisha usalama na Serikali ya Iraq katika kukabiliana na ugaidi.
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran pia amemshukuru mwenzake wa Iraq kwa "juhudi zake za kuunganisha maoni ya pande zote" katika juhudi za kuwezesha mazungumzo ya kurejesha hali ya kawaida ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Iran na Saudi Arabia na Misri mtawalia.
Amir-Abdollahian pia alikutana na Rais wa Iraq Abdul Latif Rashid baadaye mchana wa siku hiyo, ambapo Rashid alisema nchi hizo mbili zinaweza kuchangia katika kuimarisha usalama na utulivu katika eneo hilo, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Iraq.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma