

Lugha Nyingine
China yaitaka jumuiya ya kimataifa ifuatilie na kuwekeza zaidi katika suala la Somalia
Kaimu Mjumbe wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ameitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kuongeza ufuatiliaji na uwekezaji kwenye suala la Somalia.
Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Somalia Balozi Dai amesema mpito wa kisiasa na mapambano dhidi ya ugaidi nchini Somalia yamepata mafanikio, lakini hali bado ni tete, hali ya usalama haijaimarika kikamilifu, na msukosuko wa kibinadamu unatia wasiwasi.
Balozi Dai amesema ripoti ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa operesheni za kupambana na ugaidi nchini Somalia zinaweza kuwa na athari mbaya kwa hali ya kibinadamu, akisisitiza kuwa masuala kama vile kulazimishwa kujiunga na jeshi, mashambulizi holela na uharibifu wa miundombinu yanapaswa kutiliwa maanani zaidi.
Amesema China inasisitiza kuwa operesheni za kijeshi zinapaswa kuzingatia kulinda usalama wa raia hasa wanawake na watoto.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma