

Lugha Nyingine
Wang Yi akutana na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara Ulaya na Russia
Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikoministi cha China (CPC) Bw. Wang Yi, amewafahamisha waandishi wa habari kuhusu ziara yake iliyokamilika ya kutembelea katika nchi za Ulaya na Russia.
Bw. Wang amemaliza ziara yake nchini Ufaransa, Italia, Hungary na Russia na kuhudhuria Mkutano wa 59 wa Usalama wa Munich nchini Ujerumani.
Bw. Wang amesema kwenye ziara hiyo alifahamisha sera kuu za China baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na kufafanua kwa pande zote mustakabali mzuri na mchango wa kina wa ujenzi wa maendeleo ya kisasa ya China.
Kwenye suala la amani na usalama, Bw. Wang amesema China imethibitisha mara nyingi kwa ukweli kwamba njia ya kujiendeleza kwa amani si tu inatekelezeka bali pia inafanikiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma