99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Putin asema uchumi wa Russia unathibitisha uhimilivu licha ya vikwazo vya Nchi za Magharibi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2023

Watu wakiwa wameketi ndani ya mkahawa wa Star Coffee uliofunguliwa hivi karibuni, ambao ni mkahawa wenye matawi mengi uliofunguliwa kuchukua nafasi ya mikahawa ya Starbucks huko Moscow, Russia, Agosti 22, 2022. (Picha na Alexander Zemlianichenko Jr/Xinhua)

MOSCOW - Uchumi wa Russia umehimili vikwazo vya nchi za Magharibi na kustawi kwa "nguvu zaidi kuliko zilivyoamini nchi za Magharibi," Rais Vladimir Putin amesema Jumanne.

"Tumehakikisha uthabiti wa hali ya uchumi, tumelinda raia, tumeokoa ajira za watu, tumezuia uhaba wa bidhaa kwenye soko, pamoja na bidhaa muhimu, na tumeunga mkono mfumo wa kifedha na wajasiriamali," Putin amesema katika hotuba yake ya kila mwaka kwenye Mkutano Mkuu wa Russia.

Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa Pato la Taifa la Russia lilipungua kwa asilimia 2.1 Mwaka 2022, na kushinda kupungua kwa uchumi kwa asilimia 20-25 kulikokadiriwa na wachambuzi wa nchi za Magharibi mapema mwaka jana, ameeleza.

Sehemu ya Fedha za Ruble katika miamala ya kimataifa ya Russia imeongezeka maradufu ikilinganishwa na Desemba 2021. Putin amesema kwamba Moscow itaendelea kushirikiana na nchi washirika kuunda mfumo thabiti na salama wa malipo wa kimataifa usiotegemea dola ya Marekani na fedha nyinginezo za nchi za Magharibi.

"Waanzilishi wa vikwazo wanajiadhibu wenyewe. Wamechochea mfumuko wa bei katika nchi zao, kupoteza kazi, kufungwa kwa makampuni na shida ya nishati. Lakini wanawaambia raia wao kwamba Russia ndiyo wa kulaumiwa kwa kila kitu," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha