99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yasema Marekani ndiyo chanzo kikubwa zaidi cha silaha kwenye medani ya vita ya Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2023

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin Jumanne alikanusha madai ya uwongo ya maofisa fulani wa Marekani, akisema kuna ushahidi zaidi wa kutosha kuonyesha hali halisi ya Marekani kama chanzo cha matatizo badala ya "mtetezi wa amani" kwa Dunia.

Akieleza kuwa Marekani ndiyo chanzo kikubwa zaidi cha silaha kwenye medani ya vita ya Ukraine, Wang amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, jana tu, upande wa Marekani ulitangaza msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 500 kwa Ukraine.

"Inawafanya watu washangae Marekani inatafuta nini kwa madai ya uwongo kwamba China inatoa silaha, na kama Marekani inaona ni jambo la busara kuiambia Dunia kuwa inataka amani na bado inakaa na kutazama sekta yake ya ulinzi ikiweka faida mfukoni," Wang amesema.

"Sote tuliona kile ilichofanya Marekani nchini Afghanistan na mkakati wake wa 'kupigana hadi kubaki mwafghanistan wa mwisho.' Je, sasa inataka Ukraine 'ipigane hadi kubaki mwukrane wa mwisho'?" amesema.

Wang amesisitiza kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia umejengwa juu ya msingi wa kutofungamana, kutokuwa na mapambano na kutolenga upande wa tatu, jambo ambalo liko ndani ya mamlaka ya nchi yoyote mbilimbili zenye uhuru .

"Hatukubali kunyooshewa vidole na Marekani au hata mabavu yanayolenga uhusiano wa China na Russia," ameongeza.

Wang amesema, Marekani inapaswa kutafakari kwa kina juu ya kile kilichofanywa nayo, kuacha kuwasha moto au kufaidika nayo, na kubaki na nia ya dhati ya kuendeleza mazungumzo ya amani kama ambavyo China imekuwa ikifanya.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha