99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Shajara ya Uokoaji Uturuki: Tulisaidia kuokoa familia ya watu watano katika siku ya pili!

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2023

He Jun na waataalam wenzake wakifanya kazi ya uokoaji huko Uturuki. (Picha imetolewa na Kikosi cha Uokoaji cha Ramunion)

Februari 9 ni siku ya pili kwa Timu ya Uokoaji ya Ramunion kutoka China kuwa ikifanya kazi yake ya uokoaji nchini Uturuki. Bado kuna baridi kali hapa.

Tulipokea simu ya kuomba usaidizi saa 2:45 asubuhi kwa saa za hapa Alhamisi - mwanamke kutoka Mji wa Belen huko Hatay alituomba tuharakishe hadi eneo la nyumbani kwake na kuokoa familia yake iliyokuwa imefunikwa chini ya vifusi. Tulianza safari mara moja.

Picha ikionyesha ujumbe kwenye ukurasa wa Mtandao wa Twitter ukitafuta usaidizi ambao ulipokea maoni kutoka kwa mwana mtandao. (Picha ya skrini kutoka Twitter)

Dakika thelathini baadaye, tulifika katika mji huo na kukuta vifusi vya nyumba iliyobomoka vimetapakaa.

Pamoja na timu nyingine za uokoaji, tulimkuta mtu mzima na mtoto chini ya vifusi, lakini kwa bahati mbaya, hawakuwa na dalili za kuwa hai.

Vifusi na mabaki ya nyumba zilizobomoka vikionekana kwenye eneo la uokoaji Uturuki. (Picha imetolewa na Kikosi cha Uokoaji cha Ramunion)

Mji wa Belen ulikuwa ni eneo lenye majeruhi wengi. Majeruhi walipohamishwa hadi hospitalini, tuliharakisha upesi kwenda hadi mahali pengine kufanya uokoaji.

Wakati wa kutia moyo zaidi ulikuja saa 7:30 asubuhi kwa muda wa huko -- sisi na timu ya uokoaji ya Uturuki tulifanikiwa kuokoa familia ya watu wazima wawili na watoto watatu katika mji huo. Watu wazima walikuwa wameumia sana na mara moja wakasafirishwa hadi hospitalini, na kwa furaha yetu, watoto hawakuwa wamejeruhiwa.

Kuna muda wa dhahabu wa saa 72 za uokoaji kwenye eneo la tetemeko la ardhi. Tunashindana na wakati kuokoa maisha zaidi.

(Nakala hiyo imehaririwa na kutafsiriwa kutoka kwenye mahojiano na He Jun, mwanzilishi wa Timu ya Uokoaji ya Ramunion)

Waokoaji wakichimbua ardhini kwa kuzunguka katika kazi za uokoaji Uturuki. (Picha imetolewa na Kikosi cha Uokoaji cha Ramunion)

Timu ya Uokoaji ya Ramunion, pamoja na timu ya uokoaji ya Uturuki, wakisaidia kuokoa familia katika Mji wa Belen wa Hatay, Uturuki. (Picha imetolewa na Kikosi cha Uokoaji cha Ramunion)

Timu ya Uokoaji ya Ramunion, pamoja na timu ya uokoaji ya Uturuki, wakisaidia kuokoa familia katika Mji wa Belen wa Hatay, Uturuki. (Picha imetolewa na Kikosi cha Uokoaji cha Ramunion)

Timu ya Uokoaji ya Ramunion, pamoja na timu ya uokoaji ya Uturuki, wakisaidia kuokoa familia katika Mji wa Belen wa Hatay, Uturuki. (Picha imetolewa na Kikosi cha Uokoaji cha Ramunion)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha