

Lugha Nyingine
Timu ya uokoaji ya Burundi yaenda Uturuki kusaidia uokoaji wa waathirika wa tetemeko la ardhi
(CRI Online) Februari 14, 2023
Burundi imetuma timu "maalum" ya watu kumi nchini Uturuki kusaidia katika shughuli za uokoaji kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea wiki iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Bw. Albert Shingiro amesema watu hao watatumwa na mamlaka ya Uturuki katika maeneo wanayohitaji usaidizi zaidi.
Zaidi ya watu 33,000 wamefariki dunia nchini Uturuki na katika nchi jirani ya Syria ambako tetemeko la ardhi limepiga. Hata hivyo Bw. Shingiro amesema Burundi haitatuma timu nchini Syria kwa sababu ya ugumu wa kuyafikia maeneo yaliyoathirika. Habari pia zinasema raia mmoja wa Burundi ambaye alikuwa katika mji ulioathirika zaidi wa Gaziantep amehamishwa hadi mjini Ankara.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma