

Lugha Nyingine
Uturuki yakamata wakandarasi na wahandisi wanaohusika na ujenzi mbovu wa majengo kwenye eneo la tetemeko la ardhi
Watu wakisimama mbele ya vifusi vya jengo lililobomolewa kwenye tetemeko la ardhi kwenye Kahramanmaras, Uturuki Februari 12, 2023. (Picha/VCG)
Waziri wa Sheria wa Uturuki Bekir Bozdag jioni ya tarehe 12 alisema, Idara ya Mwendesha Mashtaka ya Uturuki siku hiyo ilitoa amri 134 za kukamata, zikilenga kukamata wakandarasi na wahandisi wanaohusika moja kwa moja na ujenzi mbovu wa majengo kwenye eneo la tetemeko la ardhi.
Habari kutoka chombo cha habari cha Uturuki NTV zimesema, hadi hivi sasa polisi wa Uturuki wamekamata wahusika zaidi ya 12.
Takwimu zilizotolewa na Idara ya Usimamizi wa Maafa na Mambo ya Dharura ya Uturuki tarehe 12 zimeonesha, tetemeko kubwa la ardhi lililotokea tarehe 6 Kusini mwa Uturuki limesababisha vifo vya karibu watu 30,000. Tetemeko hilo la ardhi limesababisha kubomolewa kwa majengo zaidi ya 20,000, hivyo ubora wa majengo ya makazi umetiliwa shaka na watu wa hali mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma