

Lugha Nyingine
Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China Wang Yi akutana na mshauri wa Serikali ya Nicaragua
Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na Laureano Ortega, mshauri wa masuala ya uwekezaji, biashara na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ya Rais wa Nicaragua, mjini Beijing, China, Februari 11, 2023. (Xinhua/Yao Dawei)
BEIJING - Wang Yi, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumamosi alikutana na Laureano Ortega, mshauri wa uwekezaji, biashara na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ya Rais wa Nicaragua.
Wang, ambaye pia mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amepongeza maendeleo ambayo China na Nicaragua zimepata tangu kurejesha kawaida uhusiano wa kidiplomasia zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, ushirikiano kati ya China na Nicaragua umeendelea kwa kasi, na kuzifanya nchi hizo mbili kuwa mstari wa mbele katika uhusiano wa China na Latini Amerika.
“Kurejeshwa kwa hali ya kawaida ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kunaendana na mwelekeo wa historia, kunatumikia maslahi ya watu wa pande mbili na kutafungua matarajio mapana zaidi ya maendeleo ya pande zote ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili,” amesema Wang.
Kwa upande wake Laureano Ortega amesema kuwa Nicaragua inaunga mkono kwa dhati juhudi za China za kulinda usalama wa taifa na ukamilifu wa ardhi, na inapinga kuingiliwa na nchi za nje.
Ameongeza kuwa Nicaragua inaunga mkono Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Pendekezo la Usalama wa Dunia ambayo yote yanayopendekezwa na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma