99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Matumaini yafifia kupata watu walionusurika katika tetemeko la ardhi huku idadi ya vifo ikizidi 17,000 nchini Uturuki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 10, 2023

Mhusika wa Kikosi cha Utafutaji na Uokoaji cha China akifanya shughuli ya uokoaji huko Antakya katika Jimbo la Hatay, Kusini mwa Uturuki, Februari 9, 2023. (Xinhua/Shadati)

ANKARA - Vikosi vya uokoaji vimeendelea kufanya juhudi za kila namna kutafuta watu walionusurika chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka siku ya Alhamisi, ingawa matumaini yamefifia haraka siku ya 4 baada ya matetemeko makubwa ya ardhi kuikumba Uturuki.

Idadi ya vifo kutokana na matetemeko hayo makubwa ya ardhi imeongezeka hadi 17,134 huko Uturuki, na majeruhi 71,806 hadi kufikia siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura ya Uturuki (AFAD).

Idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuongezeka zaidi punde tu juhudi za utafutaji zitakapokamilika katika eneo kubwa la majimbo 10. Wataalamu wameonya kuwa uwezekano wa kuwagundua watu walionusurika umepungua sana baada ya saa 72 kupita tangu matetemeko hayo ya ardhi yalipoikumba nchi hiyo siku ya Jumatatu wiki hii.

Waokoaji wakitafuta watu walionusurika kwenye vifusi vya jengo lililobomolewa kwenye eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi katika Jimbo la Adiyaman, Uturuki, Februari 9, 2023. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

Hata hivyo, miujiza ya kuwaokoa zaidi watu walio hai kutoka chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka zaidi ya saa 80 baada ya matetemeko hayo ya ardhi kutokea ilikuwa ya kutia moyo.

Watu wa Kikosi cha Utafutaji na Uokoaji cha China na wenzao wa Uturuki wakishirikiana kumtoa mwanamke aliyenusurika kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka huko Antakya, Jimbo la Hatay, Kusini mwa Uturuki, Februari 9, 2023. (Picha na Wang Tengfei/Xinhua)

Shirika la Utangazaji la Uturuki, TRT limeonyesha vikosi vya uokoaji vya Uturuki vikimtoa mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aitwaye Meral Nakir kutoka kwenye vifusi vya ghorofa lililobomolewa vibaya huko Malatya siku ya Alhamisi.

Bunge la Uturuki limepitisha azimio la kutekelezwa kwa hali ya dharura kwa kipindi cha miezi mitatu siku ya Alhamisi kama ilivyoombwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alisema serikali itatumia mamlaka hiyo kuzuia vitendo viovu vya baadhi ya watu, kama vile uporaji, kwenye maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi.

Huku takriban watu milioni 13.5 nchini humo wakiathiriwa na matetemeko hayo makubwa ya ardhi, Rais Erdogan alikiri kulikuwa na mapungufu katika kukabiliana na janga hilo kwa haraka katika siku ya kwanza ya maafa.

Mwanamume akilia kwa huzuni wakati waokoaji wakitafuta watu walionusurika kwenye vifusi vya jengo lililobomolewa katika tetemeko la ardhi lililotokea katika Jimbo la Adiyaman, Uturuki, Februari 9, 2023. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

Vikosi vya kimataifa vya utafutaji na uokoaji, ikiwa ni pamoja na kikosi cha waokoaji cha China chenye watu 82 na vikosi kadhaa vya kiraia, vimewasili nchini Uturuki kusaidia katika juhudi za uokoaji.

Waokoaji wakitafuta watu walionusurika kwenye vifusi vya jengo lililobomolewa katika tetemeko la ardhi lililotokea katika Jimbo la Adiyaman, Uturuki, Februari 9, 2023. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema Alhamisi kuwa watu wa utafutaji na uokoaji wapatao 6,479 kutoka nchi 56 wamewasili Uturuki kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji au kutoa msaada wa kibinadamu na matibabu, wakati vikosi vya uokoaji kutoka nchi 19 zaidi vitawasili nchini humo ndani ya masaa 24.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha