

Lugha Nyingine
China yapinga kuelezea maana ya uhusiano mzima wa China na Marekani kuwa ya ushindani pekee
BEIJING - China Jumatano imeitaka Marekani kuiona China kwa njia iliyo sahihi na yenye mantiki, kufuata sera zenye hamasa na kihalisi kwa China, na kufanya kazi na China kurudisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwenye njia tulivu ya maendeleo mazuri.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati alipojibu swali kuhusu maoni yanayohusu China kwenye hotuba ya jana Jumatano ya Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu Hali ya Taifa la Marekani.
“China siku zote inaamini kuwa uhusiano kati ya China na Marekani siyo mchezo wa kutiana hasara, haupaswi kuwa wa upande mmoja unashinda au kustawi kwa gharama ya upande mwingine,” na mafanikio ya kila upande kati yao yanatokana na fursa zake badala ya changamoto, na Dunia ni kubwa kutosha kwa nchi hizo mbili kujiendeleza na kustawi pamoja.
Amesema China haitakwepa wala kuogopa ushindani lakini inapinga kuelezea maana ya uhusiano mzima kati ya China na Marekani kuwa ya ushindani pekee, kupaka matope nchi fulani kwa kisingizio cha ushindani na kuzuia haki halali za maendeleo ya nchi nyingine, hata kwa gharama ya minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi.
Msemaji huyo ameongeza kuwa uhusiano mzuri na thabiti kati ya China na Marekani unaendana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na pia unakidhi matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.
Msemaji Mao amesema China itashughulikia uhusiano wake na Marekani kwa kufuata kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kufanya ushirikiano wa kunufaisha, na wakati huo huo China italinda kwa uthabiti mamlaka yake ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma