Kikosi cha Uokoaji cha China chawasili Uturuki
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2023
Kikosi cha Uokoaji cha China chenye watu 82 kimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Adana nchini Uturuki Februari 8, saa 10:30 alfajiri kwa saa za Ankara, baada ya kusafiri kwa ndege maalumu kwa umbali wa zaidi ya kilomita 8,000. Kiongozi wa kikosi hicho Zhao Ming amesema, kikosi hicho mara moja kimeanza kazi ya kupakua na kusafirisha mizigo, kuwasiliana na Ubalozi wa China nchini Uturuki, Serikali ya Uturuki na mashirika husika ya Umoja wa Mataifa haraka iwezekanavyo, na kuchukua jukumu maalum la utafutaji na uokoaji wa waathirika wa tetemeko kubwa la ardhi kwa kuzingatia hali ilivyo sasa ya uokoaji.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma