99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuchukua hatua za kubadili mwelekeo kabla Dunia haijaangamia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwasilisha vipaumbele vyake vya mwaka katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Februari 6, 2023. Guterres Jumatatu alitoa wito kwa nchi zote kuchukua hatua madhubuti kubadili mwelekeo kabla haijawa kuchelewa kwa Dunia kuingia kwenye maangamizi. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatatu alitoa wito kwa nchi zote kuchukua hatua madhubuti kubadili mwelekeo kabla haijawa kuchelewa kwa Dunia kuingia kwenye hatua ya maangamizi.

Wakati akiwasilisha vipaumbele vyake vya mwaka kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Guterres ametaka kuchukuliwa hatua za haraka ili kufikia amani, haki za kiuchumi na maendeleo, hatua za mabadiliko ya tabianchi, kuheshimu tofauti, na jamii jumuishi -- leo na kwa vizazi vijavyo.

Mgogoro wa Ukraine, hali ya dharura ya mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa vitisho vya nyuklia na kudhoofisha kanuni na taasisi za kimataifa kumesukuma Dunia karibu na maangamizi.

Huku akisisitiza haja ya "kusahihisha mwelekeo," mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuchukua hatua kunapaswa kuongozwa na Katiba ya Umoja wa Mataifa, nyaraka za kuanzishwa kwa shirika hilo, na Azimio la Haki za Kibinadamu la Dunia.

Katibu Mkuu huyo ametoa wito wa kuwepo kwa mtazamo wa jumla wa mwendelezo wa amani, kuchunguza vyanzo vya migogoro, na kuweka mkazo katika kuvizuia, kufanya usuluhishi, kufikia maafikiano, kujenga amani, pamoja na ushiriki zaidi wa wanawake na vijana.

Kutonana na hali ya umaskini na njaa inayozidi kuongezeka, nchi zinazoendelea zikiwa zimezama katika lindi la madeni, mifumo ya hifadhi, na usalama wa kijamii ikiwa imesambaratika, pamoja na ishara nyingine, katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kufanya mageuzi kikamilifu muundo wa mambo ya fedha ya dunia nzima.

“Dunia lazima iungane sasa kuhamasisha rasilimali, ili nchi zinazoendelea ziwe na ukwasi wa kuwekeza katika elimu, huduma za afya kwa wote, kujiandaa kwa majanga, kazi nzuri na ulinzi wa kijamii.” Amesema Guterres huku pia akitaka kupunguza utoaji hewa chafu ya kaboni na kuepuka kikomo cha Dunia cha nyuzijoto 1.5.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha