

Lugha Nyingine
China yapinga vikali hatua ya Marekani kudungua kutoka angani puto lake linalojiendesha
BEIJING - China imeeleza malalamiko makali na kupinga vikali hatua ya Marekani kutumia nguvu kushambulia puto la kiraia linalojiendesha la China, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema Jumapili katika taarifa yake.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China, Tan Kefei siku hiyohiyo ya Jumapili ameelezea kupinga vikali Marekani kushambulia kwa nguvu puto la kiraia linalojiendesha la China.
Tan amesema, shambulio hilo la Marekani lilikuwa la kuchukua hatua kupita kiasi.
"Tunapinga vikali hatua hiyo ya upande wa Marekani na tunahifadhi haki ya kuchukua hatua zinazofaa kukabiliana na hali kama hizo," Tan amesema.
Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wizara hiyo imesema, upande wa China, baada ya uhakiki, umefahamisha mara kwa mara upande wa Marekani juu ya asili ya kiraia ya puto hilo na kueleza kwamba kuingia kwake Marekani ni kwa sababu ya hali ambayo haikutarajiwa na iko nje ya uwezo kabisa.
Wizara hiyo imeeleza kuwa iliutaka upande wa Marekani kushughulikia ipasavyo jambo hilo kwa utulivu, kitaalamu na kujizuia kuchukua hatua za kupita kiasi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alisema siku ya Ijumaa alipokuwa akijibu swali husika kwamba puto hilo ni la kiraia na kwamba linatumika kwa ajili ya utafiti, hasa kwa madhumuni ya hali ya hewa. Likiwa limeathiriwa na uelekeo wa upepo na uwezo mdogo wa kujiendesha, puto hilo lilikengeuka mbali na mwendo wake uliopangwa.
Na Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani pia alieleza kuwa puto hilo halina tishio la kijeshi au kimwili kwa watu walio chini.
Chini ya hali kama hizi, utumiaji wa nguvu wa Marekani ni hatua za kupita kiasi na ukiukaji mkubwa wa mazoea ya kimataifa. Taarifa hiyo imesema, na kuongeza kuwa China italinda kwa uthabiti haki na maslahi halali ya kampuni inayohusika, na kuhifadhi haki ya kuchukua hatua zaidi ikiwa ni lazima.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma