

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu Li Keqiang ampongeza Waziri Mkuu mpya wa New Zealand Chris Hipkins
Tarehe 31, Januari, Waziri Mkuu wa serikali ya China Li Keqiang aliongea kwa njia ya simu na Waziri Mkuu mpya wa New Zealand Chris Hipkins akimpongeza kuapishwa kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya New Zealand.
Katika pongezi yake Li alisema kuwa, China na New Zealand zote ni nchi muhimu kwenye eneo la Asia-Pasifiki, na pande hizo mbili ni wenzi muhimu wa ushirikiano. Katika miaka ya hivi karibuni iliyopita, uhusiano kati ya China na New Zealand umepata maendeleo mazuri, ushirikiano kati yao kwenye sekta mbalimbali umeleta manufaa kwa watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa kikanda. Uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na New Zealand umeendelea kwa zaidi ya miaka 50, na umefikia mwanzo mpya wa kihistoria, ambapo pande hizo mbili zinatakiwa kufanya juhudi kwa pamoja, kushikilia moyo wa kujitahidi kuchukua nafasi ya kwanza, kuimarisha mawasiliano na hali ya kuaminiana, kupanua mabadilishano na kuhimiza ushirikiano, ili kusukuma mbele uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya China na New Zealand.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma