

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang afanya mazungumzo kwa njia ya simu na wenzake wa Uholanzi, Saudi Arabia na Argentina
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Qin Gang amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na wenzake wa Uholanzi, Saudi Arabia na Argentina.
Akizungumza na mwenzake wa Uholanzi Bw. Wopke Hoekstra, Bw. Qin Gang amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano na Uholanzi kwenye sekta mbalimbali na kulinda kwa pamoja mazingira ya biashara ya kimataifa.
Kwenye mazungumzo kati yake na mwenzake wa Saudi Arabia Bw. Faisal bin Farhan Al Saud, Bw. Qin amesema China inatarajia kushirikiana na Saudi Arabia katika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Kilele kati ya China na Nchi za Kiarabu, kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na nchi za kiarabu yenye mustakabali wa pamoja, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.
Alipozungumza na mwenzake wa Argentina Bw. Santiago Cafiero, Bw. Qin amesema China na Argentina zinapaswa kusukuma mbele ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na China inaiunga mkono Argentina katika kubeba wajibu mkubwa zaidi kwenye mambo ya kikanda na kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma